Lushoto inasifika kwa mandhari ya utulivu kimazingira, uwepo wa bidhaaa nyingi za mazao ya vyakula na biashara, utaliii unaovutia wazawa na wageni toka nchi nyingi duniani, viumbe na mimea adimu. Inajivunia uwepo wa historia na utamaduni wa wenyeji wa muda mrefu Wasambaa kwa upande wa kabila; wakiwa na Falme yao chini ya viongozi Mbegha, Kinyashi na Mtemi Kimweri, kwenye makao yake huko Vuga mpaka mwaka 1862. Pia wamisionari wa kutoka ulaya Wajerumani, Wa-Irish ambao wameshiriki kwa kuweka mifumo ya elimu na uinjilishaji. Lushoto inatoa elimu ya msingi hadi vyuo vikuu. Chuo cha Mahakama-IJA, Chuo cha Elimu Maalum - SEKOMU, na Chuo cha Wananchi Magamba. Elimu ya sekondari inawakilishwa na shule nyingi chini ya serikali na taasisi za kidini. Lushoto imepanuka na kuwa nyumbani kwa watanzania wote wanaoishi ama kufanya kazi.
Kijiografia ipo kwenye safu za milima ya Usambara Magharibi. Uoto wa asili vijito, milima, misitu na mabonde ni mandhari nzuri inayovutia utalii wa ndani na nje ya nchi. Misitu imekuwa mahali pa elimu/utafiti na ni zao la biashara. Mininga na Mivule ni kati ya hifadhi adimu na zawadi kwa nyanda hizi zenye karibu ya mita 1,524 toka usawa wa bahari. Safu hizi za milima zinajumuisha Usambara Mashariki ikianzia kilomita kadha kwenye tambarare za pwani (bahari ya hindi) kuelekea Usambara Magharibi kuelekea safu za milima ya upareni na kuishia Mlima Kilimannjaro. Umbali wa safu za Usambara ni kilomita 90 na upana wa 30-50 kilomita za mraba. Hali ya hewa inastawisha miti ya mbao, mazao kama kahawa, ndizi, muhogo, miwa, matunda ya aina mbali mbali na mboga mboga za aina zote kwa wingi.
Wakati wote wa mwaka Lushoto imekuwa kimbilio la wenyeji wake walioko mikoani na wageni kufika kutembea na kujipumzisha katika utulivu wa sehemu hizi nchini Tanzania. Nyumba nzuri zipo kuwapa watu nafasi hiyo kila mmoja kwa uwezo wake kifedha. Sehemu nzuri za vyakula zinapatikana katika mji wa Lushoto. Shughuli za kitalii zaweza patikana kwa urahisi kwa mawasiliano ya kielektroniki au kwa simu.
Lugha zinazotumika zaidi ni Kiswahili, Kisambaa, Kipare, Kimbugu, Kichaga, Kiha, Kihehe, Pamoja na Kingereza, Kijerumani na Kifaransa - kwa wageni wa lugha hizo.
Lushoto inafahamika zaidi kibiashara na kitamaduni. Historia na utalii wake, vyenye utajiri wa kimataifa vinapata nafasi kemkem za kutangazwa. Nia ya visionlushoto ni juhudi zitakazochangia kuweka hayo na mengine kwenye uwanja mpana kwa fanaka ya siku za usoni.
https://www.tanzaniatourism.go.tz/destination/usambara-mountains
"Lushoto kumetulia sana tofauti na miji mingine. Nimefurahia sana mapumziko yangu ya mwiisho wa mwaka. Imeniletea kumbukumbu ya siku za nyuma niliposoma huku milimani" - Yosefu
"Mandhari ya Lushoto, hewa safi na joto la wastani, matunda na vyakula vya kila aina vitakufanya uipende hii sehemu. Kila mwaka mimi na ndugu zangu tumetembelea Lushoto. Wazazi wetu walitupeleka tangu tukiwa wadogo kwenda kutembea na kujipumzisha" - Khalid
"Mimi na familia yangu 👪 tulifurahia sana muda wetu Lushoto. Watoto walifurahia safu za milima na kijani kilichokolea" - Mama Kiliani
Vision Lushoto itatoa nafasi ya kuwakaribisha wadau wa Lushoto na wageni kupata mawasiliano na huduma nyeti katika nyanja mbalimbali.
"VL" itakupa nafasi kuita na kuunganishwa kihuduma na wadau wenyeji na wakazi, taasisi na sehemu muafaka mgeni ama mwenyeji angependa kufaidika.
https://www.tripadvisor.com/Tourism-g1152711-Lushoto_Tanga_Region-Vacations.html
TAAZIZIMIZA:
Ni kikundi kinachoburudisha kwa nyimbo zenye maudhui ya kusifu, kuasa, kuburudisha jamii kwa lugha ya Kisambaa. Taazizimiza wamevunja rekodi ya nyimbo zilizopigwa kwa njia ya sauti Wilayani Lushoto kwa lugha ya Kisambaa mwaka 2017. Mbunifu wa kikundi hicho ni mzaliwa wa Lushoto, Kitongoji cha Kitivo kwa jina la Machambo Josephine R. Mahonge. Taazizimiza wametoa album yao katika mifumo miwili; Sauti na video. Machambo Josephine amekuwa mwimbaji wa muziki tangu akiwa Nyumbani, Shule ya Msingi, Sekondari na kwaya Kanisani kuanzia miaka ya 1980. Ndoto yake ilikuwa siku moja atengeneze kikundi kitakachoshirikisha umma sanaa hii. Mwanamuziki aliyechochea ari hiyo alimtaja kuwa Bwana Francis Sostenesi maarufu kama Sosi au Fula wa Lushoto, kitongoji cha Mheeo (Mhelo - Kiswahili). Kipaji chake kilimvutia sana Machambo na kutamani siku moja kuwa naye kwenye jukwaa la sanaa. Taazizimiza inaundwa pia na wasanii Maria, Pili, Bomoa,aliweza kutimiza ndoto yake. Kwa sasa andalizi lingine liko mbioni. Machambo anatumaini kuamsha ari ya kutangaza tamaduni zetu, kwa kujivunia lugha na vipaji Mungu alivyotujalia.
MNCCA ni kifupi cha Milimani, Nature, Conservation and Camping Adventure.
Kikundi hiki ni wadau waasisi wa Vision Lushoto wakijishughulisha na kuitangaza Lushoto katika nyanja za utafiti kwa mimea na viumbe wanaopatikana Lushoto, kuwaunganisha watalii wa ndani na nje ya nchi kwa wadau wa Lushoto - sehemu za mapumziko, hoteli na maeneo ya utalii. Waanzilishi wa MNCCA ni wazawa wa Magamba - Lushoto, kitongoji cha Mshaimle. Waanzilishi hawa ni pamoja na
👨🎓Andrew Kombo 👩🎓Victoria Kombo 👩🎓Felistas Mashui 👩🎓Florence Kombo 👨🎓Revocatus Hiza
Kwa mawasiliano au maulizo zaidi tuma barua pepe visionlushoto@gmail.com
***Muhimu: ✍👇Kopi hii ni hifadhi ya kumbukumbu ya mwaka 2011
https://meetingpointtanga.files.wordpress.com/2017/02/tanga-tourism-guide_2011.pdf
MAJI HAYAFUATI MKONDO / AGAINST THE CURRENT ni riwaya ya kipekee katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza, iliyoandikwa na mwandishi wa kike Mzigwa Felistas Richard Mahonge inayozungumzia changamoto anazokumbana nazo mwanamke katika kufikia ndoto za maisha yake. Mama Sinta, Sinta na Mercy ni wahusika ambao mwandishi anawatumia katika kuonesha mchango wa mwanamke katika kuijenga familia kimaadili na kiuchumi. Wahusika hawa wanachorwa na mwandishi kama wanawake wenye utashi mkubwa wa kupambanua mambo pamoja na ujasiri mkubwa katika kupambana na changamoto mbali mbali zinazojitokeza katika maisha yao. Kwa kutumia wahusika hawa na wengine, mwandishi anasisitiza suala la umuhimu wa wazazi kushiriki kwa pamoja katika kulea watoto na kuijenga familia kwani ndio mhimili wa taifa lenye uadilifu. Mwandishi anapiga vita wazazi na walezi ambao wanashiriki kwa makusudi katika kuangamiza kizazi kipya. Anakemea suala la matumizi ya madawa ya kulevya, biashara ya binadamu pamoja na rushwa. Suala la kumtanguliza Mungu katika maisha ya kila siku pamoja na thamani ya elimu katika kuwakomboa vijana kiuchumi hasa wa kike limejadiliwa pia katika riwaya hii. Mwandishi asisitiza umuhimu wa vyombo vya dola katika kusimamia haki za wanaodhulumiwa katika jamii.
Dkt Mzighwa Felistas ni mwandishi wa kike wa Kitanzania. Ni mzaliwa wa kijiji cha Mbuzii wilayani Lushoto mkoani Tanga. Ni mdau muasisi wa vision Lushoto. Amesoma shule za msingi Kitopeni, Hazina na Mhelo wilayani Lushoto kisha akapata elimu ya sekondari shuleni Popatlal Tanga. Alisoma astashahada ya ualimu chuoni Korogwe kisha akajiunga na chuo cha Mpwapwa na kufanya stashahada ya ualimu akijikita katika masomo ya lugha ya kingereza na kiswahili. Mwaka 2002 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kusoma shahada ya ualimu na kujikita katika somo la Kiswahili isimu pamoja na fasihi ya kiswahili na kiingereza. Alifanya pia shahada ya uzamili katika masuala ya elimu hususani maswala ya uongozi na utawala chuoni hapo. Alijiendeleza zaidi kitaaluma kwa kusoma shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Moi, Eldoret nchini Kenya na kuzama zaidi katika uwanja wa Fasihi. Dkt. Felistas amefundisha somo la lugha ya Kiswahili pamoja na Kiingereza katika shule mbalimbali za msingi na sekondari nchini Tanzania. Kwa sasa ni mhadhiri katika Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Ni mwandishi wa mashairi ‘I wonder!”, “What a Task” na “The Treasure” yaliyoko ndani ya kitabu kiitwacho Tell Me Friends the Riddle of the Ages (2004). Kwa sasa anaandaa kitabu chake kingine cha Siku Saba za Mwendawazimu.
Zipo huduma zifuatazo katika ubunifu wa kuwapa ajira vijana katika maeneo ya Lushoto. Kwa vijana walio tayari kujifunza na kushiriki kujiongezea kipato waweza wasiliana na vision lushoto kwa nafasi za shughuli kama:
Usafirishaji bidhaa/mizigo
Kujifunza na hatimae kutumia mashine ya kutengeneza matufali ya kupachika kwa biashara ama hata nyumba binafsi, kutumia mashine ya kutengeneza bidhaa za miti/mbao na samani, kupata ushauri nasaha kwa majifunzo na shughuli za ufundi umeme, kuchomelea, makenika n.k.
Waanzilishi wa hili kwa manufaa ya vijana wa lushoto ni Mashui & Kiango wenyeji wa Lushoto na washiriki wa visionlushoto.
HUDUMA NYINGINE AMBAZO VIJANA WANAWEZA KUZIPATA NI :
Waanzishi wa huduma hizi kwa manufaa ya vijana ni Dkt Mzighwa Felistas, Machambo Josephine, Koiya Florence, Mandela Revocutus, Mboza Antonia, Nkunde Felistas, Madafa Victoria, Mahasani Antonia na Ukuta Andrew.
Tamaduni zetu zajivunia mavazi na uzalendo wa kimila
Vitenge Kanga, na vazi la Kichwani
Kwa kutumia ubunifu na talanta vazi la kitamaduni ni tanashati na maridadi
Ni ZA kupendeza .....na maridadi
Tuma ombi ukutanishwe na mshonaji wa vazi upendalo
Agiza ubunifu wako wa mtindo upendao
Shiriki kujitangaza ufaidike na uitangaze Lushoto yetu 🎙📣
Karibuni/Welcome,
🐒🌳🍎🌽🍠🐤🌾🥀👣👣💓💖🍃🥑🍌🍏🍐🍑🍻🍷
Jionee uwanda wa Usambara Magharibi na utajiri wa nchi yetu Tanzania.
Piga simu muda wowote +255662550119 ama tuandikie 👉visionlushoto@gmail.com
Better yet, see us in person! contact us so you can meet real people, explore and receive best services from
Open today | 09:00 am – 05:00 pm |
Copyright Sheukindo Augustine Madafa Mahonge @2019 visionlushoto - All Rights Reserved.
Powered by GoDaddy